TIGblogs TIG | TIGblogs GROUP TIGBLOGS LOGIN SIGNUP
Miguel's Blog
Miguel's Blog
MAPENZI
Translations available in: English (original) | French | Spanish | Italian | German | Portuguese | Swedish | Russian | Dutch | Arabic

Ni jambo lisilo eleweka kamwe. Je, mna habari kwamba hamna "UTUMWA WENYE MATESO MENGI KULIKO UTUMWA WA KIMAPENZI"? Mbona tusijihami dhidi ya misisimko? Kwa kuwa ni jambo la kuudhi sana mtu anapojihusisha na mapenzi ambayo kwayo hayana msingi dhabiti.
Sijui iwapo nitakuwa kweli nikuwasilisha ujumbe kwa kuyanakili haya kuwa embe mbivu huliwa kwa uvumilivu?
Pindi tu baada ya usuhuba kuonyesha ishara za kunawiri kama mumea uliotiwa samadi ndipo bahari ikaanza kuchafuka. Jameni mbona hili swala sio rahisi kulipuuza kama ilivyo kawaida kupuuza maswala mengine.
Leugim ameelewa kuwa ya Mungu ni makuu na ya kuku ni Mayai.
Uhusianao dhabiti kama alivyofahamu Leugim ulizolota kiasi cha haja.
Binti aliyemdhani kuwa dhahabu kumbe kawa adhabu. Punde baada ya haya kutokea Leugim aogelea katika bahari ya luja(Depression), ninalodhihirisha wazi kuwa aliyewachwa kaachiwa mengi. Leugim hana suluhu hata kukabiliana na pigo hili. Kwa sasa kwake Leugim amani imefunga milango na kutupa funguo kusiko fikika kamwe.
Kuvunjika kwa usuhuba dhabiti ni maradhi kwa aliyeachwa.
maumivu haya yabainisha upungufu wa taaluma ya utabibu, kwani hata matabitu hawana mbinu mwafaka ya kukabiliana nao.
Nitaendelea..............................

April 9, 2008 | 3:59 AM Comments  5 comments

Tags:
You must be logged in to add tags.


Comments

bumbuwazed R Kahendi
April 10, 2008 | 1:37 AM

heheh! na umesema ukweli tu.
mapenzi ni mateso.

haya basi, si uendelee kusimulia hadithi..
daateku .
April 10, 2008 | 2:07 AM

Hilo ni jambo la kuvunjaroho na kuudhi lakini kipenda roho hula nyama mbichi.Tukiyatafakari hayo endelea kutusimulia hadithi....
daateku .
April 17, 2008 | 7:10 AM

matabitu watakuwaje na mbinu mwafaka ya kukabiliana nao? Hawawezi kamwe kwani mambo ya mapenzi ni magumu na humpata yeyote bila mpaka au kubagua awe maskini ua tajiri,wasomi na wasiosoma,vijana au wazee;Kumbuka hata paka mzee hunyua maziwa......

Suluhu ni kuwa aliyetumbukia kwa utumwa huu kujitoa mwenyewe kwani mabo ya watu wawili ni vigumu kuingilia kati.

Yatafakari hayo kisha uendelee kutusimulia.....
kikenya Miguel
April 17, 2008 | 11:30 AM
Mapenzi. Kuna watu na Viatu!!!
Yaonekana kuwa wafuatilia zaidi. Hongera
bumbuwazed R Kahendi
June 17, 2008 | 6:20 PM

Pole sana kwa kutojibu mapema.
Endelea kuandika, ndugu yangu. Umebarikiwa na kipaji cha uandishi. Lazima uendelee kukikuza. =D
Miguel's Profile

Miguel's Friends


Latest Posts
MAPENZI

Monthly Archive
January 2008
April 2008

Change Language


Tags Archive
motherlanguageday

Friends
angel
Brenda
Gudina Fufa Yadeta
Kaanaeli Kaale
Miora Raf
Mpasua Msonobari


4927 views
Important Disclaimer