TIGblogs TIG | TIGblogs GROUP TIGBLOGS LOGIN SIGNUP
Miguel's Blog
Miguel's Blog


MAPENZI
Translations available in: English (original) | French | Spanish | Italian | German | Portuguese | Swedish | Russian | Dutch | Arabic

Ni jambo la lisilo eleweka kamwe. Je, mna habari kwamba hamna "UTUMWA WENYE MATESO MENGI KULIKO UTUMWA WA KIMAPENZI"? Mbona tusijihami dhidi ya misisimko? Kwa kuwa ni jambo la kuudhi sana mtu anapojihusisha na mpendwa ambaye kwa kweli amcheza shere.
Sijui iwapo nitakuwa kweli nikuwasilisha hili kuwa embe mbivu huliwa kwa uvumilivu?
Pindi tu baada ya usuhuba kuonyesha ishara za kunawiri kama mumea uliotiwa samadi ndipo bahari ikaanza kuchafuka. Jameni mbona hili swala sio rahisi kulipuuza kama ilivyo kawaida kupuuza maswala mengine.
Leugim ameelewa kuwa ya Mungu ni makuu na ya kuku ni Mayai.
Uhusianao dhabiti kama alivyofahamu Leugim ulizolota kiasi cha haja.
Binti aliyemdhani kuwa dhahabu kumbe kawa adhabu. Punde baada ya haya kutokea Leugim aogelea katika bahari ya luja(Depression), ninalodhihirisha wazi kuwa aliyewachwa kaachiwa mengi. Leugim hana suluhu hata kukabiliana na pigo hili. Kwa sasa kwake Leugim amani imefunga milango na kutupa funguo kusiko fikika kamwe.
Kuvunjika kwa usuhuba dhabiti ni maradhi kwa aliyeachwa.
maumivu haya yabainisha upungufu wa taaluma ya utabibu, kwani hata matabitu hawana mbinu mwafaka ya kukabiliana nao.
Nitaendelea..............................

April 9, 2008 | 3:59 AM Comments  5 comments

Tags:




Miguel's Profile

Miguel's Friends


Latest Posts
MAPENZI

Monthly Archive
January 2008
April 2008

Change Language


Friends
angel
Gudina Fufa Yadeta
Kaanaeli Kaale


2121 views
Important Disclaimer